Monday, 30 June 2014

KOMBE LA DUNIA BRAZIL 2014




Add caption
              Zimefika fainali nyingine za Kombe la Dunia na safari hii zitafanyika nchini Brazil kuanzia Ijumaa ya Juni 12 2014. Kama kawaida washambuliaji wa timu zitakazoshiriki fainali hizo watakwenda kupambana kwa dhamira moja ya kuonyesha uhodari wa kutikisa nyavu na kuinyakua tuzo hiyo binafsi.
Orodha ya Mastraika mahiri ni pamoja na Mario Balotelli wa Italia, Robin van Persie wa Uholanzi na Karim Benzema wa Ufaransa na wakali hao watakuwa kwenye vita hiyo kali kumsaka bingwa wa Kiatu cha Dhahabu kwenye Kombe la Dunia.
Makala haya yanazungumzia mastaa wanaopewa nafasi kubwa zaidi ya kukinyakua kiatu hicho cha dhahabu kama wataanza michuano hiyo wakiwa kwenye viwango vyao vya siku zote ambazo vimewafanya kuwa mahiri zaidi wanapokuwa ndani ya uwanja.
Sergio Aguero
Licha ya kusumbuliwa na hali ya kuwa majeruha , straika huyu wa Argentina ni hatari anapolikaribia goli. Aguero ni aina ya washambuliaji ambaye timu nyingi zingependa kuwa na huduma yake uwanjani. Staa huyo alifunga mabao 28 katika mechi 34 alizochezea mabingwa wa Ligi Kuu England, Manchester City.
Hivyo kama straika huyo ataendelea kuwa kwenye kiwango hicho kwa mechi zote kwenye fainali hizo za Kombe la Dunia, huku kikosini Argentina akiwa na uhakika wa kupata pasi za mwisho kutoka kwa Lionel Messi na Angel Di Maria, hilo litamweka kwenye nafasi nzuri ya kufunga mabao mengi. 
Neymar
Mwanzo wake klabuni Barcelona umekumbana na nyakati nyingi ngumu na kushindwa kuonyesha makali yake halisi, lakini kwenye Kombe la Dunia, Neymar atakuwa na kitu tofauti cha kukifanya ndani ya uwanja.
Staa huyo anapewa nafasi kubwa ya kulibeba taifa la Brazil ambalo ni wenyeji wa fainali hizo na alianza kuonyesha makali yake ya kutikisa nyavu kwenye mchezo wa kirafiki wa ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Panama.
Kama Brazil ya Luiz Felipe Scolari itakuwa kwenye ubora wake na Neymar akawa staa wao kwenye safu ya ushambuliaji, strika huyo mwenye umri wa miaka 22 ana nafasi kubwa ya kuwa mshindani wa kweli kwenye vita hiyo ya kuwania Kiatu cha Dhahabu.

Said PiePie, Nairobi

No comments:

Post a Comment