![]() |
| Mashabiki wa timu ya taifa ya Brazil |
Timu 32 zinashiriki katika mashindano hayo yatakayodumu kwa wiki nne zijazo na maelfu ya mashabiki kutoka kila pembe ya dunia wameshawasili nchini Brazil kufuatilia moja kwa moja mechi hizo.
Brazil imetumia dola bilioni 11 kuandaa mashindano hayo jambo ambalo limezua malalamiko makubwa miongoni mwa raia wengi wa nchi hiyo. Kumeshuhudiwa maandamano makubwa hasa katika sekta ya uchukuzi. Usalama umeimarishwa kote nchini humo huku kiasi ya wanajeshi na askari 150,000 wakishika doria. Huku macho yote yakielekezwa Brazil, rais wa shirikisho la soka duniani FIFA Sepp Blatter amedokeza kuwa ananuia kutafuta muhula mwingine wa kuhudumu kama rais wa FIFA licha ya madai ya ufisadi yanayolizonga shirikisho hilo.
Said PiePie,Nairobi.

No comments:
Post a Comment