Monday, 30 June 2014

KOMBE LA DUNIA BRAZIL 2014




Add caption
              Zimefika fainali nyingine za Kombe la Dunia na safari hii zitafanyika nchini Brazil kuanzia Ijumaa ya Juni 12 2014. Kama kawaida washambuliaji wa timu zitakazoshiriki fainali hizo watakwenda kupambana kwa dhamira moja ya kuonyesha uhodari wa kutikisa nyavu na kuinyakua tuzo hiyo binafsi.
Orodha ya Mastraika mahiri ni pamoja na Mario Balotelli wa Italia, Robin van Persie wa Uholanzi na Karim Benzema wa Ufaransa na wakali hao watakuwa kwenye vita hiyo kali kumsaka bingwa wa Kiatu cha Dhahabu kwenye Kombe la Dunia.
Makala haya yanazungumzia mastaa wanaopewa nafasi kubwa zaidi ya kukinyakua kiatu hicho cha dhahabu kama wataanza michuano hiyo wakiwa kwenye viwango vyao vya siku zote ambazo vimewafanya kuwa mahiri zaidi wanapokuwa ndani ya uwanja.
Sergio Aguero
Licha ya kusumbuliwa na hali ya kuwa majeruha , straika huyu wa Argentina ni hatari anapolikaribia goli. Aguero ni aina ya washambuliaji ambaye timu nyingi zingependa kuwa na huduma yake uwanjani. Staa huyo alifunga mabao 28 katika mechi 34 alizochezea mabingwa wa Ligi Kuu England, Manchester City.
Hivyo kama straika huyo ataendelea kuwa kwenye kiwango hicho kwa mechi zote kwenye fainali hizo za Kombe la Dunia, huku kikosini Argentina akiwa na uhakika wa kupata pasi za mwisho kutoka kwa Lionel Messi na Angel Di Maria, hilo litamweka kwenye nafasi nzuri ya kufunga mabao mengi. 
Neymar
Mwanzo wake klabuni Barcelona umekumbana na nyakati nyingi ngumu na kushindwa kuonyesha makali yake halisi, lakini kwenye Kombe la Dunia, Neymar atakuwa na kitu tofauti cha kukifanya ndani ya uwanja.
Staa huyo anapewa nafasi kubwa ya kulibeba taifa la Brazil ambalo ni wenyeji wa fainali hizo na alianza kuonyesha makali yake ya kutikisa nyavu kwenye mchezo wa kirafiki wa ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Panama.
Kama Brazil ya Luiz Felipe Scolari itakuwa kwenye ubora wake na Neymar akawa staa wao kwenye safu ya ushambuliaji, strika huyo mwenye umri wa miaka 22 ana nafasi kubwa ya kuwa mshindani wa kweli kwenye vita hiyo ya kuwania Kiatu cha Dhahabu.

Said PiePie, Nairobi

Thursday, 12 June 2014

KIPUTE CHA KOMBE LA DUNIA BRAZIL 2014


Mashabiki wa timu ya taifa ya Brazil
          Mashindano ya kombe la dunia yanaanza rasmi hii leo nchini Brazil. Wenyeji watamenyana na Croatia baadaye leo jioni katika mechi ya ufunguzi itakayochezwa katika uwanja wa michezo wa Sao Paulo. Kocha wa Brazil Luiz Felipe Scolari amewahimiza raia wa nchi hiyo kuwaunga mkono wachezaji wao wanapoanzisha azma yao ya kulinyakua kombe la dunia.
Timu 32 zinashiriki katika mashindano hayo yatakayodumu kwa wiki nne zijazo na maelfu ya mashabiki kutoka kila pembe ya dunia wameshawasili nchini Brazil kufuatilia moja kwa moja mechi hizo.
          Brazil imetumia dola bilioni 11 kuandaa mashindano hayo jambo ambalo limezua malalamiko makubwa miongoni mwa raia wengi wa nchi hiyo. Kumeshuhudiwa maandamano makubwa hasa katika sekta ya uchukuzi. Usalama umeimarishwa kote nchini humo huku kiasi ya wanajeshi na askari 150,000 wakishika doria. Huku macho yote yakielekezwa Brazil, rais wa shirikisho la soka duniani FIFA Sepp Blatter amedokeza kuwa ananuia kutafuta muhula mwingine wa kuhudumu kama rais wa FIFA licha ya madai ya ufisadi yanayolizonga shirikisho hilo.

Said PiePie,Nairobi.

Wednesday, 11 June 2014

KOMBE LA DUNIA BRAZIL 2014



               
Strika mahiri wa timu ya Brazil Naymer Junior

   Michuano ya Kombe la Dunia itafanyika nchini Brazil Juni 12,2014. Kama kawaida mastrika   wa timu zitakazoshiriki fainali hizo watakwenda kupambana kwa dhamira moja ya kuonyesha uhodari wa kutikisa nyavu na kuinyakua tuzo hiyo binafsi.Kwenye orodha ya Mastraika mahiri ni pamoja na  Mario Balotelli wa Italia, Robin van Persie wa Uholanzi na Karim Benzema wa Ufaransa na wakali hao watakuwa kwenye vita hiyo kali kumsaka bingwa wa Kiatu cha Dhahabu kwenye Kombe la Dunia.

Lionel Messi
Mambo hayakuwa mazuri msimu uliopita kwenye kikosi cha Barcelona, lakini siku zote Lionel Messi hafundishwi kufunga. Anazijua nyavu vizuri sana na kwamba ndiye atakayeongoza mashambulizi ya Argentina kwenye fainali hizo za Kombe la Dunia za Brazil.
Kwenye kundi lao, Argentina ipo pamoja na timu za Bosnia-Herzegovina, Iran na Nigeria na timu hizo hazionekani kuwa ngumu kiasi cha kumzuia Messi asifunge. Kuna hatari kubwa kwamba huenda Messi akamaliza vita yake ya kuwania Kiatu cha Dhahabu kwenye mechi hizo za hatua ya makundi pekee.Sergio Aguero
Aguero ni aina ya washambuliaji ambaye timu nyingi zingependa kuwa na huduma yake uwanjani. Staa huyo alifunga mabao 28 katika mechi 34 alizochezea mabingwa wa Ligi Kuu England, Manchester City.
Hivyo kama straika huyo ataendelea kuwa kwenye kiwango hicho kwa mechi zote kwenye fainali hizo za Kombe la Dunia, huku kikosini Argentina akiwa na uhakika wa kupata pasi za mwisho kutoka kwa Lionel Messi na Angel Di Maria, hilo litamweka kwenye nafasi nzuri ya kufunga mabao mengi.
Neymar
Katika  klabu ya Barcelona umekumbana na nyakati  ngumu na kushindwa kuonyesha makali yake halisi, lakini kwenye Kombe la Dunia, Neymar atakuwa na kitu tofauti cha kukifanya ndani ya uwanja.
Staa huyo anapewa nafasi kubwa ya kulibeba taifa la Brazil ambalo ni wenyeji wa fainali hizo na alianza kuonyesha makali yake ya kutikisa nyavu kwenye mchezo wa kirafiki wa ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Panama.
Kama Brazil ya Luiz Felipe Scolari itakuwa kwenye ubora wake na Neymar akawa staa wao kwenye safu ya ushambuliaji, fowadi huyo mwenye umri wa miaka 22 ana nafasi kubwa ya kuwa mshindani wa kweli kwenye vita hiyo ya kuwania Kiatu cha Dhahabu.

Luis suarez
Luis Suarez alitajwa kuwa mshambuliaji hatari zaidi barani Ulaya kwa msimu uliopita, lakini kwenye Kombe la Dunia kwa sasa anapambana na muda kupona maumivu yake baada ya kufanyiwa upasuaji wa goti mwezi uliopita.
Lakini, kama atacheza fainali hizo basi bila shaka mabao yatamfuata na Uruguay itakuwa kwenye nafasi nzuri zaidi ya kufanya vizuri. Kwenye fainali zilizopita za Kombe la Dunia zilizofanyika Afrika Kusini, Uruguay ilikomea nusu fainali, lakini mwaka huu kama Suarez atakuwa fiti na kuongoza safu ya ushambuliaji sambamba na Edinson Cavani, basi mabingwa hao wa Amerika Kusini watatamba na Suarez atatimiza ndoto zake.

Cristiano Ronaldo
Staa huyu wa Real Madrid atakwenda kwenye fainali hizo akiwa kwenye kiwango safi akitokea kutwaa ubingwa wa Ligi ya Mabingwa Ulaya na kuweka pia rekodi ya mabao.
Fowadi huyo alifunga mabao 51 katika mechi 47 za michuano yote aliyocheza klabuni Real Madrid kwa msimu wa 2013-14. Huku akiwa mshindi wa Tuzo ya Fifa ya Ballon d’Or, Ronaldo ndiye anayebeba matumaini ya Ureno katika fainali hizo za Kombe la Dunia, hivyo ni lazima afunge mabao kuibeba timu hiyo.
Kama hilo la kufunga mabao atalifanya vizuri basi moja kwa moja atakuwa ameingia kwenye kinyang’anyiro cha kukinyakua Kiatu cha Dhahabu cha Fifa kwenye Kombe la Dunia.

Said PiePie, Nairobi


SIMBA NA YANGA ZANYEMELEA WACHEZAJI WA KENYA



Mshambulizi matata wa timu ya Gor Mahia Dan Serenkuma.

       Timu za Tanzania Simba  na Yanga zimesema zitanunua wachezaji wawili wa kigeni nje ya nchi. Yanga inamfikiria straika wa Uganda anayecheza Gor Mahia,Dan Sserunkuma na imeshazungumza nae.
Lakini Simba nayo kocha wake, Zdravko Logarusic amezungumza na wachezaji watatu wa humu nchini akiwemo, Rama Salim wa Gor Mahia.
habari zilizofikia meza ya taarifanews zinasema kwamba Simba wamezungumza na wachezaji wawili wa Uganda na muda wowote watasafiri nchini Tanzania.
Lakini AFC Leopards  imeingia kwenye kinyang’anyiro na kusaka saini za Danny na Rama ambao wote wana mikataba.Patrick Ngaira ambaye Mwenyekiti msaidizi wa AFC amenasema wachezaji wanaoweza kujaza nafasi ya Allan Wanga na tunahisi kuwa Sserunkuma ni mmoja wao. Rama vile vile ni mzuri na ushirikiano wake na Sserunukma unaweza kutufaa.

Said PiePie,Nairobi