Wednesday, 11 June 2014

KOMBE LA DUNIA BRAZIL 2014



               
Strika mahiri wa timu ya Brazil Naymer Junior

   Michuano ya Kombe la Dunia itafanyika nchini Brazil Juni 12,2014. Kama kawaida mastrika   wa timu zitakazoshiriki fainali hizo watakwenda kupambana kwa dhamira moja ya kuonyesha uhodari wa kutikisa nyavu na kuinyakua tuzo hiyo binafsi.Kwenye orodha ya Mastraika mahiri ni pamoja na  Mario Balotelli wa Italia, Robin van Persie wa Uholanzi na Karim Benzema wa Ufaransa na wakali hao watakuwa kwenye vita hiyo kali kumsaka bingwa wa Kiatu cha Dhahabu kwenye Kombe la Dunia.

Lionel Messi
Mambo hayakuwa mazuri msimu uliopita kwenye kikosi cha Barcelona, lakini siku zote Lionel Messi hafundishwi kufunga. Anazijua nyavu vizuri sana na kwamba ndiye atakayeongoza mashambulizi ya Argentina kwenye fainali hizo za Kombe la Dunia za Brazil.
Kwenye kundi lao, Argentina ipo pamoja na timu za Bosnia-Herzegovina, Iran na Nigeria na timu hizo hazionekani kuwa ngumu kiasi cha kumzuia Messi asifunge. Kuna hatari kubwa kwamba huenda Messi akamaliza vita yake ya kuwania Kiatu cha Dhahabu kwenye mechi hizo za hatua ya makundi pekee.Sergio Aguero
Aguero ni aina ya washambuliaji ambaye timu nyingi zingependa kuwa na huduma yake uwanjani. Staa huyo alifunga mabao 28 katika mechi 34 alizochezea mabingwa wa Ligi Kuu England, Manchester City.
Hivyo kama straika huyo ataendelea kuwa kwenye kiwango hicho kwa mechi zote kwenye fainali hizo za Kombe la Dunia, huku kikosini Argentina akiwa na uhakika wa kupata pasi za mwisho kutoka kwa Lionel Messi na Angel Di Maria, hilo litamweka kwenye nafasi nzuri ya kufunga mabao mengi.
Neymar
Katika  klabu ya Barcelona umekumbana na nyakati  ngumu na kushindwa kuonyesha makali yake halisi, lakini kwenye Kombe la Dunia, Neymar atakuwa na kitu tofauti cha kukifanya ndani ya uwanja.
Staa huyo anapewa nafasi kubwa ya kulibeba taifa la Brazil ambalo ni wenyeji wa fainali hizo na alianza kuonyesha makali yake ya kutikisa nyavu kwenye mchezo wa kirafiki wa ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Panama.
Kama Brazil ya Luiz Felipe Scolari itakuwa kwenye ubora wake na Neymar akawa staa wao kwenye safu ya ushambuliaji, fowadi huyo mwenye umri wa miaka 22 ana nafasi kubwa ya kuwa mshindani wa kweli kwenye vita hiyo ya kuwania Kiatu cha Dhahabu.

Luis suarez
Luis Suarez alitajwa kuwa mshambuliaji hatari zaidi barani Ulaya kwa msimu uliopita, lakini kwenye Kombe la Dunia kwa sasa anapambana na muda kupona maumivu yake baada ya kufanyiwa upasuaji wa goti mwezi uliopita.
Lakini, kama atacheza fainali hizo basi bila shaka mabao yatamfuata na Uruguay itakuwa kwenye nafasi nzuri zaidi ya kufanya vizuri. Kwenye fainali zilizopita za Kombe la Dunia zilizofanyika Afrika Kusini, Uruguay ilikomea nusu fainali, lakini mwaka huu kama Suarez atakuwa fiti na kuongoza safu ya ushambuliaji sambamba na Edinson Cavani, basi mabingwa hao wa Amerika Kusini watatamba na Suarez atatimiza ndoto zake.

Cristiano Ronaldo
Staa huyu wa Real Madrid atakwenda kwenye fainali hizo akiwa kwenye kiwango safi akitokea kutwaa ubingwa wa Ligi ya Mabingwa Ulaya na kuweka pia rekodi ya mabao.
Fowadi huyo alifunga mabao 51 katika mechi 47 za michuano yote aliyocheza klabuni Real Madrid kwa msimu wa 2013-14. Huku akiwa mshindi wa Tuzo ya Fifa ya Ballon d’Or, Ronaldo ndiye anayebeba matumaini ya Ureno katika fainali hizo za Kombe la Dunia, hivyo ni lazima afunge mabao kuibeba timu hiyo.
Kama hilo la kufunga mabao atalifanya vizuri basi moja kwa moja atakuwa ameingia kwenye kinyang’anyiro cha kukinyakua Kiatu cha Dhahabu cha Fifa kwenye Kombe la Dunia.

Said PiePie, Nairobi


No comments:

Post a Comment